Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Ndg. Naysan Sahba, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhamasishaji Duniani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo Mei 3, 2023. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Spika na mgeni
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Ndg. Naysan Sahba, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhamasishaji Duniani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo Mei 3, 2023.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Spika na mgeni wake wamejadili namna bora ya kushirikiana katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
Aidha katika ziara hiyo Ndg. Sahba aliambatana na Bi.Shalini Bahuguna Mwakilishi Mkazi wa UNICEF -Tanzania na Bi. Angela Travis, Mshauri wa Mawasiliano wa shirika hilo katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *